Bingwa mara mbili wa dunia na Olimpiki Faith Kipyegon amevunja rekodi ya dunia ya umbali wa maili moja katika mkondo wa monaco Diamond league nchini Ufaransa ,Ijumaa usiku.
Kipyegon aliziparakasa mbio hizo kwa dakikd 4 sekunde 7 nukta 64 akivunja rekodi ya mwaka 2019 yake Sifan Hassan wa Uholanzi ya dakika 4 sekunde 12 nukta 33.
Ilikuwa rekodi ya tatu ya dunia kwa Kipyegon mwenye umri wa miaka 29 chini ya miezi miwili,baada ya kuvunja rekodi za mita 1500 akiweka rekodi mpya ya dakika 3 sekunde 49 nukta 11 Juni 2 katika mashindano ya Florence Diamond League na kisha kuvunja rekodi ya mita 5,000 katika mashindano ya Paris Diamond League akiandikisha rekodi mpya ya dakika 14 sekunde 5 nukta 20.