Fainali za CHAN kuandaliwa kati ya Februari 1 na 28 mwakani

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya nane ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani maarufu kama CHAN yataandaliwa baina ya Februri mosi na 28 mwaka ujao .

Haya yameafikiwa kwenye mkutano wa baraza kuu la shirikisho la kandanda barani Afrika CAF ulioandaliwa Jumatatu jijini Nairobi.

Raundi ya kwanza ya mechi za kufuzu kwa CHAN itaandaliwa kati ya Oktoba 21 na 27 na raundi ya mwisho iandaliwe Disemba mwaka huu.

Timu 13 zitakazofuzu zitajiunga na wenyeji Tanzania,Uganda na Kenya kwa kipute cha mwakani.

Rais wa CAF Dkt Patrice Motsepe pia ametangaza kuwa zawadi ya pesa kwa mabingwa wa makala ya mwaka ujao imeongezwa kama njia ya kuyafanya kuwa na msisimko zaidi.

Awali Motsepe kwenye ziara yake alikagua ujenzi na ukarabati wa viwanja vya Kasarani na Talanta City votakavyoandaa michuano ya CHAN na mapema Jumatatu alikutana na Rais William Ruto, aliyekariri kujitolea kwa Kenya kuandaa fainali za kufana za CHAN na pia AFCON mwaka 2027.

Dkt Motsepe aliahidi kurejea nchini Disemba mwaka huu kukagua ujenzi wa viwanja na miundo mbinu.

Ni mara ya kwanza kwa Rais Motsepe kuandaa kikao cha kamati kuu ya CAF jijini Nairobi

Share This Article