Makala ya 35 ya fainali za kuwania kombe la AFCON yataandaliwa nchini Morocco kati ya Disemba 21 mwaka 2025 na Januari 18 mwaka 2026.
Shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF) liliafikia uamuzi huo jana katika kikao maaluma klichoongozwa na kinara wake Dkt Patrice Motsepe.
Pia CAF ilitangaza kuahirisha fainali za kuwania kombe la Afrika kwa wanawake WAFCON, kutoka mwaka huu hadi mwaka ujao kuanzia Julai 5 na 26.