Fahamu kuhusu programu mpya ya Gava Mkononi

Tom Mathinji
2 Min Read

Wakenya sasa watanufaika pakubwa na huduma 5,000 za serikali kupitia mfumo wa dijitali wa e-Citizen, baada ya serikali kuzindua programu ya Gava Mkononi.

Huku taifa hili likishuhudia kuimarishwa kwa uunganishwaji wa intaneti katika maeneo ya mashinani pamoja  na mijini, programu mpya ya Gava Mkononi ambayo imezinduliwa na serikali, itawanufaisha pakubwa wakenya kwa kupata huduma za serikali kupitia simu za rununu.

Uzinduzi wa programu ya Gava Mkononi umezingatia kuwa wakenya wengi sasa wana simu za kisasa almaarufu, smartphones na hivyo kurahisisha utumizi wake.

Kinyume na vituo vya  Huduma Centers, ambavyo vinapatikana katika makao makuu ya kaunti, Gava Mkononi sasa inapatikana hata katika maeneo ya mashinani.

Huduma ya Gava Express itatekelezwa kwa ushirikiano na sekta ya kibinafsi na inalenga kufungua zaidi ya vituo  300,000 kote nchini.

Ufanisi huu ni sehemu ya hatua zilizopigwa na taifa hili katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwa njia ya dijitali tangu serikali ya Kenya Kwanza ilipochukua hatamu za uongozi.

Wakati wa sherehe za siku kuu ya Jamhuri mwaka 2022, Rais William Ruto aliahidi kuwa huduma 5,000 za serikali zitapatikana kwa mtandao wa E-Citizen platform,kurahisisha utoaji huduma, ukusanyaji wa mapato, kuimarisha uwazi na kutokomeza ufisadi.

Kufikia mwezi Januari mwaka huu, kulikuwa na huduma mpya 391 katika mtandao wa e-Citizen.

Huduma kumi bora katika mtandao wa e-Citizen ni pamoja na:

NTSA – Utoaji wa leseni za kuendesha gari.

Huduma za kusajili biashara.

Hati ya Maadili kutoka huduma ya polisi.

Usajili wa Hati za ndoa.

Usajili wa Rais wa kigeni.

Huduma za uhamiaji.

Halmashauri ya bandari nchini.

Halmashauri ya ukusanyaji ushuru.

HELB

Hazina ya hustler.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *