Fahamu kuhusu kipute cha EURO mwaka 2024

Dismas Otuke
2 Min Read

Mataifa 24 yatashiriki makala ya 17 ya fainali za kuwania kombe la Euro nchini Ujerumani, kuanzia Ijumaa hii Juni 14 hadi Julai 14.

Mabingwa mara tatu Ujerumani wataandaa fainali hizo katika viwanja 10 vilivyo katika miji 10 tofauti.

Mechi za makundi zitaandaliwa kati ya Juni 14 na 26 huku hatua ya mwondoano ikichezwa kuanzia Juni 29.

Timu 24 zilizofuzu kwa kipute hicho zimetengwa katika makundi sita, huku timu mbili bora kutoka kila kundi na timu nne bora zitakazomaliza katika nafasi ya tatu zikijikatia tiketi kwa mwondoano.

Kundi A: Switzerland, Scotland, Hungary, and Germany

Kundi B: Albania, Croatia, Italy, and Spain

Kundi C: England, Denmark, Serbia, and Slovenia

Kundi D: France, Austria, Poland, and the Netherlands

Kundi E: Ukraine, Slovakia, Romania, and Belgium

Kundi F: Portugal, Georgia, Turkey, and the Czech Republic

Mchuano wa ufunguzi utaandaliwa Ijumaa hii kaunzia saa nne usiku kati ya Ujermani na Scotland, katika uwanja wa Munich unaoselehi mashabiki 60,000.

Fainali itaandaliwa Julai 14 katika uga wa Olympiastadion,mjini Berlin wenye uwezo wa kumudu mashabiki 71,000.

Viwanja 9 kati ya 10 vitakavyoandaa makala ya mwaka huu ni vile vilivyoandaa fainali za kombe la Dunia mwaka 2006.

Ujerumani na Uhispania ndio mataifa yenye ufanisi zaidi kwenye fainali hizo yakiwa na mataji matatu kila moja, wakati Italia na Ufaransa zikinyakua kombe hilo mara mbili kila moja.

Mataifa sita ya Jamhuri ya Czech,Uholanzi,Ugiriki,Ureno,Denmark na Urusi yamenyakua kombe moja kilamoja.

Mechi hizo zitaandaliwa saa kumi alasiri,saa moja jioni na saa nne usiku mida ya Afrika Mashariki.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *