Timu ya Uhispania imefuzu kwa fainali ya kipute cha kuwania kombe la Bara Ulaya kinachoendelea nchini Ujerumani.
Uhispania ilifuzu kwa fainali hizo, kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Ufaransa katika nusu fainali.
Bao la Ufaransa lillitiwa kimiani na Randal Kolo Muani katika dakika ya nane.
Lamine Yamal alisawazisha kisha Dani Olmo akafunga la pili dakika ya 21 na 25 mtawalia, na kuipa Uhispania ushindi huo.
Nusu fainali nyingine itasakatwa hii leo Jumatano saa nne usiku kati ya Uingereza na Uholanzi.