Esther Musila ashukuru wasichana waliomwacha Gurdian Angel

Marion Bosire
1 Min Read

Esther Musila mke wa mwanamuziki Gurdian Angel ameshukuru wasichana ambao waliwahi kuwa kwenye mahuasiano ya kimapenzi na Gurdian awali na kisha kumwacha.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Clouds Media jijini Dar es Salaam nchini Tanzania Esther alisema waliomwacha mwimbaji huyo walimpa mume kwa hivyo anawashukuru.

Kando na hilo, Esther alielezea kwamba alifikisha umri wa miaka 50 ndipo akapata ujazo wa maisha kama alivyokuwa akitaka kupitia kwa kumpata Gurdian Angel.

Musila amemzidi Gurdian umri lakini anasema jinsi anampenda anahisi kwamba yeye ndiye wa umri mdogo kuliko Gurdian.

Gurdian ambaye jina lake halisi ni Peter Omwaka kwa upande wake alisema kwamba alipompata Esther akili yake ilifunguka na maisha yake yakabadilika kabisa.

Alisema hapo ndipo alifahamu kwamba kuna mengi mazuri maishani zaidi ya kuwa tu mtu maarufu.

Wawili hao pamoja na wasaidizi wao wako nchini Tanzania kwa ajili ya kuandaa video ya wimbo ambao Gurdian amemshirikisha mwimbaji wa Tanzania Obby Alpha uitwao “Pigana na Mungu”.

Share This Article