EPRA: Kampuni ya gesi ya Embakasi ilihudumu bila leseni

Tom Mathinji
2 Min Read

Mamlaka ya kudhibiti Kawi nchini (EPRA),  imefichua kuwa kampuni iliyohusika katika mlipuko wa gesi eneo la Embakasi Alhamisi usiku, iliendesha shughuli zake bila leseni.

Kwa mujibu wa EPRA, kampuni hiyo ilituma maombi ya kupewa kibali cha kujenga kiwanda cha gesi mara tatu, tarehe 19 mwezi Machi, tarehe 20 mwezi Juni na tarehe 31 mwezi Julai, lakini Maombi hayo yalikataliwa.

“Sababu kuu ya kukataliwa kwa maombi hayo ni kushindwa kuafikia umbali wa kiusalama unaohitajika. EPRA ilibaini kuwepo kwa msongamano mkubwa wa watu karibu na eneo lililopendekezwa, huku mmiliki wa kiwanda hicho akitakiwa  kuwasilisha tathmini ya hatari ya Ubora (QRA) inayoonyesha maelezo ya tahadhari iwapo kutatokea  mlipuku,” ilisema EPRA kupitia taarifa Ijumaa.

Aidha kwa mujibu wa  EPRA, kampuni hiyo ilishindwa kuwasilisha tathmini ya hatari ya Ubora (QRA) ambayo inaonyesha maelezo ya mlipuko kama ule uliotokea tarehe moja mwezi February saa sato na nusu usiku.

EPRA imeelezea kuwa maelezo ya milipuko huundwa kupitia programu ya tarakilishi na huonyesha madhara ya mlipuko na hutumika kutathmini usalama kwenye maeneo yaliyo karibu.

“Aliyetuma maombi hayo hakutoa chetincha QRA, hatua iliyosababisha kusababisha kukataliwa kwa maombi hayo. Alitumiwa barua pepe zilizotoa sababu za kukataliwa,” iliongeza halmashauri hiyo.

Swali linalowakuna wengi vichwa ni jinsi kampuni hiyo ilivyokwepa sheria zote na pia vyombo vya sheria kuanzisha kituo hicho haramu licha ya hatua kali za kiutawala za EPRA za kudhibiti mitambo haramu inayofanya kazi nchini.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

TAGGED:
Share This Article