Ekwee Ethuro ateuliwa mwenyekiti wa HELB

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amemteua Ekwee Ethuro kuwa mwenyekiti wa halmashauri inayosimia mikopo ya masomo ya elimu ya juu HELB .

Ethuro alikuwa spika wa kwanza wa bunge la Senate kuanzia mwaka 2013 na awali alihudumu kama Mbunge wa Turkana ya kati baina ya mwaka 2008 hadi 2013.

Kupitia kwa gazeti rasmi la serikali Ethuro ameteuliwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Septemab 19.

Ethuro anarejea kuongoza HELB baada ya kuteuliwa mwaka 2018 na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Share This Article