Ekiru apigwa marufuku kwa ulaji muku

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa mbio za Milano marathon mwaka 2021 Titus Ekiru, amepigwa marufuku na kitengo cha maadili ya wanariadha AIU.

Ekiru anakabiliwa na makosa manne ya matumizi ya dawa zilizoharamishwa ambayo endapo yatathibishwa yote, atapigwa mafufuku ya miaka 10.

Ekiru aliye na umri wa miaka 31, aliandikisha historia mei 26 mwaka 2021 kuwa mwanaume wa pili baada ya Eliud Kipchoge,kutimka mbio za kilomita 42 chini ya saa 2 na dakika 3 aliposhinda Milano marathon kwa saa 2 dakika 2 na sekunde 57.

Mwanariadha huyo alishiriki mashindanoni kwa mara ya mwisho Novemba 26 mwaka 2021 aliposhinda mbio za Abu Dhabi Marathon.

Ekiru ni mwanariadha wa hivi punde kupigwa marufuku kwa makosa ya ulaji muku nchini, huku shirikisho la riadha ulimwenguni na shirika la kupambana na ulaji muku ulimwenguni WADA likikaza kamba dhidi wanariadha wadanganyifu.

Website |  + posts
Share This Article