Umoja wa Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS imeiwekea vikwazo Niger kufuatia jaribio la mapinduzi ya serikali.
Kulingana na taarifa ya pamoja ya ECOWAS kufuatia kikao cha pamoja cha mataifa ya Afrika Magharibi, Niger imewekewa vikwazo kadhaa vikiwemo kufunga kwa anga zote za kuingia na kutoka nchini humo, kufunga mipaka yote ya Niger na kufunga akaunti zote za pesa zinazomilikiwa na Niger katika ECOWAS.
Umoja huo umeelezea kuwa utajaribu kutumia kila mbinu kurejesha hali ya utulivu nchini Niger.