Ebwali Boys na Madira Soccer Assassins ndio mabingwa wa mashindano ya Safaricom Chapa Dimba kaunti Vihiga.
Timu hizo mbili ndizo za kwanza kufuzu kwa fainali ya mashindano ya Safaricom Chapa Dimba katika eneo la magharibi.
Ebwali iliwazabua Bunyore Assasins magoli 4-1 kupitia penalti kufuatia sare tasa katika fainali iliyoandaliwa jana Jumapili katika uwanja wa Mumboha eneo la Luanda kaunti ya Vihiga.
Katika fainali ya wasichana, Madira Soccer Assassins walitawazwa mabingwa kufuatia ushindi wa goli 1 kwa bila dhidi ya Maroo Queens.