EACC kuzindua mpango wa utendakazi wa mwaka 2023-2028

Tom Mathinji
1 Min Read

Tume ya Maadili na Kupambana na ufisadi, EACC itazindua mpango wa miaka mitano wa kutoa mwongozo kuhusu utekelezaji wa majukumu yake.

Mpango huo wa mwaka 2023-2028, utazinduliwa katika Jumba la Mikutano ya Kimataifa la Jomo Kenyatta KICC.

Hafla ya uzinduzi itaongozwa na Waziri Mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi.

Mkutano huo wa uzinduzi utawaleta pamoja mwenyekiti wa EACC Dkt. David Oginde, Afisa Mkuu Mtendaji Twalib Mbarak, majaji, mawaziri, wabunge na magavana miongoni mwa wadau wengine.

Mpango huo ulibuniwa kupitia mashauriano ya wadau kutokana na mfumo wa sasa wa ufisadi pamoja na yale tume hiyo ilijifunza kutoka kwa mpango wa awali wa mwaka 2018-2023 uliokamilika mwezi Juni mwaka huu.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article