Tume ya maadili na kupambana na ufisadi hapa nchini EACC, imeanza kuwahoji wakurugenzi 39 na manaibu wao wa idara mbali mbali katika serikali ya kaunti ya Busia, kwa madai ya kuajiriwa kwa misingi ya kikabila.
Kupitia kwa barua rasmi, tume hiyo imewataka wakurugenzi hao kufika katika afisi zake mjini Bungoma kutoa habari kuhusu jinsi waliajiriwa.
Shughuli ya kuwaajiri wakurugenzi hao iliibua hisia kali kutoka kwa wakazi wa kaunti ya Busia.
Mwakilishi wa wadi ya Bukhayo kaskazini/Walatsi Gadi Jakaa, aliwasilisha hoja katika bunge la kaunti hiyo akitaka uchunguzi ufabywe kuhusu jinsi wakurugenzi hao walivyoajiriwa.
Kulingana na Jakaa, uajiri wa wakurugenzi hao umedhihirisha kuwepo kwa ukabila na ubaguzi katika serikali ya kaunti hiyo.