Dulla Makabila ajiombea msamaha kwa Mungu wakati huu wa Ramadhani

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Tanzania Dulla Makabila amemwomba mwenyezi Mungu msamaha mapema wakati huu anaendelea kuadhimisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama muumini wa dini ya Kiisilamu.

Mwimbaji huyo wa mtindo wa “Singeli” alitumia akaunti yake ya mtandao wa Instagram kuhusu jinsi anavyopata mijarabu wakati huu wa mfungo.

Anaelezea kwamba amekuwa akiitiwa tamasha mbalimbali ila anakataa kwa sababu ya mwezi mtukufu lakini kama njia ya kumshawishi, waandalizi wa tamasha hizo wanaongeza malipo watakayompa.

Msanii huyo anasema kwamba anakataa kazi hizo lakini pale nyumbani anaombwa pesa za kuandaa chakula cha kufuturu na kwamba kufikia sasa ameitwa kutumbuiza kwenye tamasha sita na bado zinazidi kuongezeka.

Mwisho anaonekana kukubali mshawasha huo kinyume cha masharti ya Ramadhani lakini anaomba msamaha akisema, “Mungu nisamehe kipaji umenipa mwenyewe.”

Website |  + posts
Share This Article