Droo ya mchujo kufuzu kwa AFCON 2025 kuandaliwa Februari 20

Dismas Otuke
1 Min Read

Droo ya kufuzu kwa makala ya 35 ya pashika ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2025, itaandaliwa Jumanne Februari 20 jijini Cairo Misri.

Droo hiyo itashirikisha mataifa manane yaliyo katika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa FIFA yakiwa Somalia,Djibouti, Sao Tome, Chad, Mauritius,Sudan Kusini, Liberia na Eswatini.

Michuano hiyo itachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini kati ya tarehe 18 na 26 mwezi ujao, huku washindi wa jumla wakifuzu kwa hatua ya makundi .

Jumla ya mataifa 48 yatajumuishwa katika makundi 12 huku timu mbili kutoka kila kundi zikijikatia tiketi kwa makala ya mwaka 2025 ya kindumbwendumbwe cha AFCON.

Share This Article