Droo ya Ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho Afrika, kuandaliwa leo, Qatar

Dismas Otuke
1 Min Read

Droo ya mechi za mwondoano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la shirikisho barani Afrika itaandaliwa leo usiku mjini Doha, Qatar.

Timu nane zilizosalia katika kila taji zitabaini wapinzani wao wa kwota na nusu fainali huku mkondo wa kwanza na wa pili wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ukiandaliwa kati ya Aprili mosi na 8 mwaka huu.

Robo fainali za kombe la shirikisho zitapigwa baina ya April 2 na 9 mwaka huu.

Ligi ya mabingwa itawashirikisha mabingwa watetezi Al Ahly SC ya Misri, Al Hilal (Sudan), AS FAR (Morocco), Espérance Sportive de Tunis (Tunisia), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Orlando Pirates (Afrika Kusini), Pyramids (Egypt), na MC Alger (Algeria).

Timu zilizosalia katika kombe la shirikisho zinajumuisha mabingwa watetezi Zamalek SC (Misri), Asec Mimosas (Cote d’Ivoire), Al Masry (Misri), CS Constantine (Algeria), RS Berkane (Morocco), Simba SC (Tanzania), Stellenbosch FC (Afrika Kusini), na USM Alger (Algeria).

Washindi wa Ligi ya mabingwa watatuzwa shilingi milioni 520, huku washindi wa kombe la shirikisho wakipokea milioni 260.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *