Droo ya Kombe la Dunia kuandaliwa Disemba 5 Washington DC

Mechi zitachezwa katika miji 16 tofauti nchini Marekani, Mexico na Canada.

Dismas Otuke
1 Min Read

Droo ya fainali za Kombe la Dunia kwa wanaume itaandaliwa Disemba 5 mwaka huu mjini Washington DC nchini Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump na kinara wa soka duniani Gianni Infantino, wametangaza haya katika Ikulu ya White House.

Droo hiyo itaandaliwa katika kituo cha Kennedy.

Mataifa 48 yatakayoshiriki dimba hilo, ikiwa idadi kubwa kwa mara ya kwanza, yatashuhudia timu hizo zikitengwa katika makundi 12.

Mechi zitachezwa katika miji 16 tofauti nchini Marekani, Mexico na Canada.

Michuano ya 104 ya kindumbwendumbwe hicho itaandaliwa kati ya Juni 11 huku fainali ikisakatwa Julai 19 mjini New York.

Website |  + posts
Share This Article