Droo ya fainali za Kombe la Dunia baina ya vilabu mwaka ujao nchini Marekani, itaandaliwa leo mjini Miami .
Timu 32 zilizofuzu zitabaini wapinzani katika droo hiyo ambayo kwa mara ya kwanza itashirikisha idadi hiyo vilabu.
Afrika inawakilishwa na Mabingwa Al Ahy kutoka Misri,Esperance ya Tunisia, Wydad Casablanca ya Morocco na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini .
Bara Asia linawakilishwa na mabingwa Al Hilal ya Saudi Arabia, Urawa Red Diamonds ya Japan,Al Ain ya Milki za Kiarabu na Ulsan Hyundai ya Korea Kusini.
Ulaya iliyo na timu nyingi zaidi inajumuisha mabingwa Real Madrid,Manchester City,Bayern Munich,Borusia Dortmund, Inter Milan,Chelsea,Benfica,FC Porto,Atletico Madrid, Juventus,Paris St Germain na RB Salzburg.
Amerika ya kati na kaskazini ina Pachuca , Monterrey, Club Leon, Inter Miami, Seattle Sounders na Auckland City.
Amerika Kusini ina Botafogo,Flamingo Fluminense,Palmeiras,Boca Juniors na River Plate.
Viwanja 12 nchini Marekani vitatumika kuandaa mechi 63 za kipute hicho, kati ya Juni 15 na Julai 13 mwaka ujao.