Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza kuandaa droo ya makala ya nane ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), Januari 15 katika ukumbi wa KICC,Nairobi.
Fainali hizo zimeratibiwa kufanyika kati ya tarehe 1 na 28 mwezi ujao katika mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania.
Jumla ya nchi 19 zitashiriki kipute cha mwaka huu ambacho kwa mara ya kwanza kitaaandaliwa kwa pamoja na nchi tatu.
Ni mara ya kwanza kwa Kenya kufuzu kwa fainali hizo ambao huandaliwa kila baada ya miaka miwili .
Kenya itaandaa mechi zake katika viwanja vya Kasarani na Nyayo, huku Police Sacco na Ulinzi Complex vikitumika kwa maozezi.
Senegal ndio mabingwa watetezi baada ya kuwashinda Algeria mabao 5-4 kupitia mikiki ya penati kufuatia sare ya 2-2.
Kenya ambao watajumuishwa kundi Kundi A watacheza mechi ya ufunguzi Februari Mosi,huku Uganda ikijumuishwa kundi B nao Tanzania wakiwa kundi C.