DPP akataa kumwachilia Waititu kwa dhamana

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) Renson Ingonga, amekataa kata kata kumwachilia Gavana wa zamani wa Kiambu, Ferdinand Ndungu Waititu, kwa dhamana akisubiri rufaa yake katika mahakama ya kuu.

Ingonga amekataa ombi hilo la kumwachilia Waititu kwa dhamana akisisitiza kuwa ameshtakiwa na kupatikana na hatia ya kesi ya ufisadi ambayo amehukumiwa kifungo cha miaka 12 au kulipa faini ya shilingi milioni 53.

Serikali imekataa ombi la mawakili wa Waititu kudai kuwa hukumu hiyo itamaliza amali yake ya kisiasa ya zaidi ya miaka 20 ikisema sio sababu tosha.

Ingonga amesema Waititu hajatimiza vigezo vinavyohitajika ili kuachiliwa kwa dhamana kusubiri rufaa.

Jaji Lucy Njuguna wa mahakama ya Milimani, alimpata Waititu na hatia kwa kesi ya ufisadi na anatarajiwa kuamua kesi ya rifaa tarehe 3 mwezi ujao.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *