Dorcas Rigathi kuhutubia Kongamano la Wajane barani Afrika

Martin Mwanje & OSDP
1 Min Read

Mkewe Naibu Rais Dorcas Rigathi leo Alhamisi atahutubia Kongamano la Wajane barani Afrika litakaloandaliwa Zanzibar, Tanzania.

Maudhui ya kongaman hilo ni “Wanawake katika Ujane: Kufanyia Marekebisho Nafasi ya Afrika.”

Miongoni mwa mambo mengine, kongamano hilo linalenga kuangazia masuala mbalimbali yanayowaathiri wajane barani Afrika na kutoa wito wa kufanywa kwa maekebisho ya kimuundo kuhusiana na namna serikali zinavyofanya kazi.

Nchini Kenya, mkewe Naibu Rais amekuwa mstari wa mbele kutetea haki za wajane huku akitekeleza miradi inayolenga kuwainua wajane kiuchumi katika kaunti za Nairobi, Kajiado, Migori, Laikipia, Kakamega, Bungoma, TransNzoia, Nandi, Bomet, Kilifi na Nakuru.

Miradi hiyo ni pamoja na ufugaji wa samaki, mbuzi na nyuki, upanzi wa miche na ushonaji wa nguo miongoni mwa mingine.

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Mkewe Mariam Mwinyi, Mkewe Rais wa Zimbabwe Auxillia Mnangagwa na aliyekuwa Mke wa Rais wa Tanzania Anne Mkapa ni miongon mwa watakaohudhuria kongamano hilo.

Martin Mwanje & OSDP
+ posts
Share This Article