Huduma zote 5,000 za serikali zinazotolewa kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la e-Citizen zinapatikana katika benki ya Equity.
Wakenya wanaweza wakanufaika na huduma hizo kwa kutumia programu ya benki hiyo kwenye simu zao za mkononi au kwa kutembelea mawakala 40,000 wa benki hiyo kote nchini.
Hii ni kwa mujibu wa Afisa Mkuu Mtendaji wa benki hiyo Dkt. James Mwangi.
“Tumeunganisha biashara na serikali,” alisema Dkt. Mwangi wakati wa uzinduzi wa programu ya Gava Mkononi katika jumba la mikutano ya kimataifa la KICC, Nairobi leo Ijumaa.
Akimwelezea Rais Ruto hatua zilizopigwa na benki hiyo katika kuweka huduma za serikali kwenye jukwaa hilo, Dkt. Mwangi alisema upatikanaji wa huduma za serikali kidijitali utasaidia pakubwa ukuaji uchumi wa nchi.