Mamlaka ya Kudhibiti Bidhaa za Mafuta na Nishati, EPRA imemteua Dkt. Joseph Oketch kuwa kaimu Meneja Mkurugenzi Mkuu kufuatia kujiuzulu kwa Daniel Kiptoo siku ya Jumamosi.
Hadi uteuzi wake, Dkt. Oketch alikuwa msimamizi nishati na umeme, akisimamia udhibiti wa viwango katika kampuni ya EPRA.
Dkt. Oketch ana tajriba ya zaidi ya miaka 25 katika sekta ya nishati na awali alikuwa amefanya kazi ya usimamizi katika kampuni ya umeme nchini, KPLC.