Djokovic atwaa dhahabu ya Olimpiki baada ya subira ya miaka 16

Dismas Otuke
1 Min Read

Sogora wa Tenisi Novak Djokovic kutoka Serbia amenyakua dhahabu ya Olimpiki kwa mara ya kwanza baada ya kumbwaga Carlos Alcaraz wa Uhispania kwenya fainali ya wanaume Jumapili jioni.

Djokovic alisajili ushindi wa seti 2-0 za 7-6 na 7-6 katika fainali hiyo akishinda taji pekee iliyomkwepa katika amali yake ya kucheza tenisi ya kulipwa.

Mserbia huyo anajiunga na Serena Williams, Rafael Nadal, Andre Agassi na Steffi Graf kama wachezaji walionyakua tuzo zote nne za Grand Slam na pia dhahabu ya Olimpiki.

Djokovic aliye na umri wa miaka 37 ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kunyakua dhahabu ya Olimpiki.

Share This Article