Mwanamuziki wa Marekani P.Diddy ambaye yuko kizuizini ameshtakiwa kwa mara nyingine kwa kile kinachotajwa kuwa ubakaji.
Jamaa fulani ambaye ni mwanamuziki ambaye huimba barabarani anasema kwamba aliwahi kuwa na kikao na Diddy ambacho kiliishia kwa yeye kubakwa.
Mwanaume huyo ambaye jina lake limebanwa anasema kwamba Diddy alimbaka mdomoni na kumwingilia pia kinyume na maumbile baada ya kumtilia dawa kwenye kinywaji.
Kulingana na stakabadhi za kesi hiyo, jamaa huyo alikuwa akiimba nje ya eneo moja maarufu la burudani huko Los Angeles Novemba 2022, wakati alialikwa kwa mojawapo ya sherehe za Diddy na jamaa aliyejitambulisha kama msaidizi wa Diddy.
Anasema alisafirishwa hadi makazi ya Diddy na kweli alifanikiwa kuonana naye akidhania kwamba angemsaidia kuendelea katika tasnia ya muziki.
Katika kikao hicho alipatiwa kinywaji na walipokuwa wakijadiliana akazungumzia uzuri wa mkufu wa Diddy na Diddy akamuuliza iwapo angependa kuona vito vyake vingine.
Jamaa huyo anaelezea kwamba aliongozwa na Diddy kueleka chumba kingine ambapo alianza kusinzia ingawa alikunywa kinywaji kimoja pekee. Alishangaa alipoona kwamba chumba hicho hakikuwa na vito na Diddy akaanzisha mazungumzo ya ngono.
Kulingana naye, dawa liyokuwa ametiliwa kwenye kinywaji ilimzidia akapoteza fahamu ambapo Diddy alitumia fursa hiyo kumbaka.
Alipopata fahamu asubuhi ya siku iliyofuata alijipata kwenye nyumba hiyo akapata jamaa mwingine akimwekea maji kwenye mshipa. Alibebwa kwenye gari akarejeshwa eneo alikotolewa nje ya eneo lile maarufu la burudani huko Los Angeles na tangu wakati huo hajawasiliana na Diddy.
Tukio hilo anasema lilimsababishia maumuvu mwilini, msongo wa mawazo na aibu na sasa ameamua kumshtaki Diddy akidai fidia.