Msanii wa kutoka Tanzania, Naseeb Abdul Issack, anayejulikana kwa jina la usanii kama Diamond Platnumz ameshinda Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Afrika kwenye Tuzo za Muziki za Ulaya za MTV (EMAs 2023).
Ndiye Msanii wa kwanza kutoka Afrika kushinda tuzo tatu za MTV EMA.
Katika kitengo hicho, Diamond aliwahsinda wasanii Asake, Burna Boy, Libianca na Tyler ICU.
Diamond Platnumz aliwahi kushinda tuzo mbili za Msanii Bora wa Afrika na mwimbaji Bora Duniani (Afrika/India) kwa usiku mmoja kwenye MTV EMA 2015.
Pia ndiye msanii wa kwanza barani Afrika kufikisha maoni milioni 900 kwenye YouTube.