Dereva wa mbunge wa Kibra atozwa faini ya shilingi laki moja

Dismas Otuke
1 Min Read

George Oduor, ambaye ni dereva wa mbunge wa Kibra Peter Orero, amefikishwa mahakamani siku ya Jumatatu na kutozwa faini ya shilingi laki moja kwa kosa la kukiuka sheria za trafiki.

Hakimu wa mahakama ya Milimani Rose Ndombi ametoa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja gerezani au faini ya shilingi laki moja kwa Oduor baada yake kukiri kukiuka sheria za barabarani.

Oduor and Walikuwa na Orero kweny gari la Prado wakipita kwa mkondo usiosatahili barabarani na kunaswa kwenye kamera ya mwanahabari wa CNN Larry Madowo.

Mbunge Orero alipoulizwa kiini cha kukiuka sheria za trafiki alionyesha ukaidi hatua ambayo imezua taharuki mitandaoni.

Aidha Oduor ameomba msamaha na akiongeza kuwa alikuwa akikimbia katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta alipotekeleza kosa hilo.

Website |  + posts
Share This Article