DCI: Jamani tusaidieni kumkamata Collins Jumaisi Khalusha

Martin Mwanje
1 Min Read
Collins Jumaisi Khalusha - Mshukiwa wa mauaji eneo la Kware, Embakasi

Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI kwa mara nyingine imetoa wito kwa Wakenya kutoa taarifa zitazosaidia katika kumkamata Collins Jumaisi Khalusha.

Khalusha ni mshukiwa mkuu wa mauaji yaliyotokea katika eneo la Kware, Embakasi mwaka jana.

“Ikiwa una taarifa yoyote kuhusu aliko Collins Jumaisi Khalusha, tunakusihi kuitoa kisiri kupitia nambari 0800722203,” imesema DCI kwenye taarifa.

DCI imetoa ikitoa wito kama huo tangu mwezi Agosti mwaka jana, ila wito huo haujazaa matunda kufikia sasa.

Jumaisi na wenzake 12 walitoroka kutoka korokoro za kituo cha polisi cha Gigiri kaunti ya Nairobi.

Watu hao 12 wanasemekana kuwa raia wa Eritrea ambao walipatikana nchini bila kibali.

Mnamo siku ya Jumanne, Agosti 20, 2024 saa 5 asubuhi, afisa wa polisi aliyekuwa kwenye zamu katika kituo cha polisi cha Gigiri kwa jina Gerald Mutuku, alizuru seli zote kama kawaida akiwa ameandamana na msimamizi wa duka la kituo hicho kuwapa washukiwa kiamshakinywa.

Walipofungua seli, walishangaa kupata kwamba hakukuwa na yeyote ndani kwani walihepa baada ya kukata nyaya za eneo wanalootea jua.

Kutokana na kisa hicho, maafisa kadhaa wa polisi wanaofanya kazi katika kituo hicho cha polisi wamesimamishwa kazi ili kuwezesha uchunguzi kufanywa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *