David Kemei ameteuliwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya ushindani nchini yaani Competition Authority of Kenya(CAK) na Rais William Ruto baada ya kuidhinishwa na Bunge.
Uteuzi huo umetengazwa jumatatu na Rais Ruto huku Kemei akimrithi Adano Rioba ambaye amekuwa kaimu Mkurugenzi Mkuu.
Kemei,anamiliki shahada ya uzamifu kutoka cjhuo kikuu cha Nairobi katika taaluma ya uhasibu .
Rais Ruto alimteua Kemei mwezi uliopita kabla ya bunge la Senate kumuidhinisha katika wadhfa huo.
Awali Kemei alikuwa mwenyekiti wa shirika la Kenya Re.