Msanii wa Nigeria Davido,na mkewe Chioma wameondoka hospitalini baada ya kujaliwa watoto pacha .
Wapenzi hao wawili walionekana kwenye picha wakiondoka katika hospitali moja nchini Marekani, siku chache baada taarifa kuzagaa kuhusu kujaliwa watoto pacha.
Tukio hilo limetajwa kama baraka maradufu baada ya kufiwa na mwanao wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu, Ifeanyi Adeleke mwishoni mwa mwaka jana
Ifeanyi alikufa maji alipokuwa akiogelea kwenye kidimbwi mwaka uliopita siku chache baada ya kuadhimisha miaka mitatu ya kuzaliwa.