Daktari apoteza uraia wa Marekani alikozaliwa

Marion Bosire
1 Min Read

Daktari Siavash Sobhani wa umri wa miaka 61 alizaliwa nchini Marekani ambako babake alikuwa anahudumu kama afsa wa ubalozi wa Iran.

Hivi maajuzi, Sobhani alituma maombi ya kupata pasipoti mpya ya usafiri na badala ya kupatiwa, akapokea barua kutoka kwa serikali iliyomjuza kwamba hakustahili kupatiwa uraia alipozaliwa.

Alikua na kusomea nchini Marekani ambapo amekuwa akihudumu kama daktari kwa miaka 30 sasa na hii ndio mara ya kwanza anapata shida ya uraia.

Serikali ya Marekani imekuwa ikithibitisha uraia wake kila mara alipokuwa akichukua pasipoti mpya ya usafiri.

Sobhani anaangazia mipango ya kustaafu na ndio maana alikuwa anatafuta stakabadhi hiyo ya usafiri maana yeye na mke wake wanapanga kusafiri hadi maeneo mbalimbali nchini wakitafuta jamii ambayo watajiunga nayo na kujenga makao huko.

Daktari huyo sasa amelazimika kutuma maombi ya mkazi wa kudumu nchini Marekani na kufikia sasa anasema ametumia pesa nyingi kwa mchakato wa kutafuta haki kisheria.

Share This Article