Dadake Juma Jux apokelewa na mashemeji Nigeria kwa mbwembwe

Marion Bosire
2 Min Read
Juma Jux na Priscilla Ojo

Dada ya mwanamuziki wa Tanzania Juma Jux amesafiri hadi Nigeria kukutana na familia ya mpenzi wa Jux aitwaye Priscilla Ojo.

Mama ya Priscilla kwa jina Iyabo Ojo ambaye ni mwigizaji maarufu nchini Tanzania alichapisha video inayoonyesha jinsi walimpokea Fatima nchini humo.

Iyabo alikuwa amejawa na furaha tele akimpokea kwenye uwanja wa ndege huku Priscilla akionekana kufutahia maua na zawadi nyingine alizoletewa.

Iyabo na Fatima wanataniana utadhani ni marafiki wa tangu zamani huku wakizungumza juu ya vile watahudhuria harusi ya JUx na Priscilla wakisema watu wa Tanzania hawako tayari kwa mbwembwe zao.

Mama huyo anaonekana akiigiza vazi la harusi akitumia karatasi za kufunga zawadi huku akicheza kwa furaha.

Priscilla anaonekana pia akijaribu kumfundisha mamake mintindo ya densi ya Tanzania akisema kwamba ataielewa kwa lazima.

Juma Jux na Priscilla wameweka uhusiano wao wa kimapenzi wazi tangu Julai, 2024 na hivi maajuzi walifichua kwamba watafunga ndoa mwakani.

” Wewe ni wifi mzuri kwa Priscilla na nyongeza ya thamani kwa familia yetu. Ukarimu wako umegusa mioyo yetu.” aliandika Iyabo kwenye Instagram.

Alimtahadharisha ajiandae kwa mambo mazuri akiwa nchini Nigeria huku akiahidi kwamba watamwonyesha mapenzi, vicheko na ziara jijini Lagos.

Jux naye alichapisha video hiyo ya mapokezi ya dadake kwa wakwe zake akirejelea waliokuwemo kuwa malkia wake.

Website |  + posts
Share This Article