Croatia imepokonywa maandalizi ya mashindano ya dunia ya mbio za nyika mwaka 2024 kutokana na utepetevu.
Shirikisho la riadha Ulimwenguni limetoa taarifa leo Ijumaa kusema kuwa miji ya Pula na Medulin nchini Croatia, haiko tayari kuandaa mashindano hayo ya dunia na itabidi mwandalizi mpya atafutwe upya.
Mwandalizi wa mashindano hayo likiwa ni taifa la Ulaya anatarajiwa kubainika kabla ya mwishoni mwezi huu wa Septemba.
Croatia ilikuwa iandae makala ya mwaka ujao mnamo Februari 10 lakini tarehe imesongezwa mbele hadi mwezi Machi.
Makala ya mwaka huu ya mbio za nyika yaliandaliwa mjini Barthurst nchini Australia.