Muungano wa Wafanyakazi nchini, COTU umepongeza nyongeza ya mshahara ya asilimia sita kwa wafanyakazi wa viwango vyote.
Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli amevitaka vyama vya wafanyakazi chini ya mwavuli wa COTU kuanza majadiliano ya nyongeza mpya ya kipindi cha miaka miwili ijayo.
Atwoli alisema haya muda mfupi baada ya Waziri wa Leba Dkt. Alfred Mutua kutangaza nyongeza hiyo ya asilimia sita.