COTU yamtaka Rais kutekeleza kikamilifu matakwa ya Gen Z

Dismas Otuke
1 Min Read

Muungano wa wafanyakazi nchini – COTU, umemtaka Rais William Ruto kutekeleza kikamilifu baadhi ya matakwa ya vijana wa Gen Z ili wasitishe maandamano ambayo yameathiri utendakazi nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa COTU Benson Okwaro amelalama kwamba  maandamano hayo yamechangia uharibifu wa mali na kuathiri wafanyakazi na ipo haja ya kusitishwa.

Ameongeza kuwa ipo haja kwa Rais Ruto kuharakisha utekelezaji wa ahadi zake kwa vijana na pia kubuni serikali isiyokuwa na mafisadi.

Naibu Katibu Mkuu huyo pia amekariri msimamo wa COTU kuwaunga mkono vijana katika jitihada zao za kupigania mabadiliko ya uongozi serikalini.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *