COTU yampongeza Ruto kwa kufutilia mbali mikataba ya Adani

radiotaifa
1 Min Read
Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli

Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi nchini, COTU umepongeza hatua ya Rais William Ruto kufutilia mbali mikataba ya uwekezaji ya kampuni ya Adani kutoka India.

Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli amesema hatua ya Rais Ruto hapo jana jioni, ilikuwa ya kijasiri na iliyojiri kwa wakati ufaao.

“Tangazo la Rais jana jioni kwenye hotuba ya pili bungeni imerejesha imani ya wafanyakazi katika sekta zote hususan wafanyakazi wa chama cha wahudumu wa viwanja vya ndege nchini (KAWU) chini ya mamlaka ya viwanja vya ndege,” alisema Atwoli

Atwoli amekariri kuwa wataendelea kufanya mashauriano kati ya vyama vya wafanyakazi, serikali na wafanyakazi ili kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Kwenye hotuba yake bungeni jana Alhamisi, Ruto alifutilia mbali mikataba ya kampuni ya Adani ya kustawisha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, JKIA na kampuni ya kusambaza umeme ya KETRACO.

Share This Article