Mabingwa watetezi wa taji la bara la Amerika Argentina, wamefuzu kwa nusu fainali ya mashindano hayo kwa kuizaba Ecuador kupitia matuta ya 4-1.
Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida.
Goli la Argentina lilifungwa na Lautaro Martínez nalo la Ecuador likapachikwa na Kevin Rodríguez dakika za 35 na 90+1 mtawalia.
Robo fainali ya pili itakuwa kati ya Venezuela na Canada hapo kesho saa kumi usiku.