Congo yathibitisha visa 28 vya Ebola

 Hali ya tahadhari imechukuliwa na serikali kuzuia maambukizi zaidi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Congo imeripoti visa 28 vipya vya mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola huku wengine 15 wakifariki Kusini Mashariki mwa Kasai.

Maafisa wa afya wamesema kuwa mmoja wa waliofariki ni mwanamke mjamzito aliyelazwa hospitalini mwishoni mwa mwezi Agosti.

Hali ya tahadhari imechukuliwa na serikali kuzuia maambukizi zaidi.

Ni mara ya 16 kwa Congo kuripoti visa vya Ebola tangu mwaka 1976 huku ugonjwa huo ukisababisha maafa ya mamilioni ya watu katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

Website |  + posts
Share This Article