Cleophas Shimanyula na azma yake ya kuongoza Kandanda Kenya

Dismas Otuke
1 Min Read

Cleophas Shimanyula ambaye ni mwenyekiti na mwanzilishi wa klabu ya Kakamega Homeboyz, ni mmoja wa waaniaji wa Urais wa shirikisho la soka nchini FKF katika uchaguzi wa Disemba 7 mwaka huu.

Shimanyula ambaye ni mfanyibiashara  katika sekta kadhaa ikiwemo ujenzi na usafiri ameiongoza timu ya Homeboyz kutwaa kombe la FKF mwaka 2023 na pia ni mojawapo wa timu zinazofanya vyema katika ligi kuu ya Kenya.

‘Toto’ anavyojulikana na wafuasi wake alizundua kampeini yake,  huku akimteua naibu mwenyekiti wa klabu ya Bandari FC ,Twaha Mbarak kuwa mwaniaji mwenza wake.

Baadhi ya ajenda kuu kwenye manifesto yake Shimanyula ni kuweka mbinu mwafaka za kutafuta na kutambua talanta ili kuwa na timu za taifa bora,kushirikiana na serikali ili kukakikisha upatikanaji wa raslimali za ujenzi wa viwanja vya kukuza soka tokea mashinani,na kuleta uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa kandanda.

Shimanyula pia amepata uungwaji mkono kutoka kwa mwakilishi wa zamani wa FKF magharibi ya Kenya,Andrew Amukowa.

Toto aliibuni timu ya Homeboyz mwaka 2010  na miaka mitatu baadaye ikapandishwa ngazi kucheza Ligi kuu kwa mara ya kwanza  mwaka 2013.

Homeboyz ilitwaa ubingwa wa kombe la FKF na kuiwakilisha Kenya katika kombe la shirikisho Afrika.

Website |  + posts
Share This Article