Mwigizaji wa Uganda Claire Nampala amefunga ndoa na jamaa kwa jina Joseph Kyambadde nchini Marekani.
Hafla yao ilihudhuriwa na raia kadhaa wa Uganda wanaoishi Marekani.
Nampala alisafiri hadi Marekani mwaka 2019 kwa ajili ya tamasha la filamu la Afrika ambako filamu yake kwa jina “Forbidden” ilikuwa imeteuliwa kuwania tuzo.
Tangu wakati huo hajarejea nchini Uganda na haijulikani iwapo anaendeleza kazi zake za uaandaaji filamu pamoja na uigizaji.
Mwaka 2022 aliripotiwa kufuzu kutoka taasisi ya utabibu ya Ultimate iliyoko Florida ambako alisomea usimamizi katika sekta ya afya.
Sio mengi yanafahamika kuhusu Joseph Kyambadde zaidi ya kwamba yeye ni mfanyabiashara.