Chuo Kikuu cha Rongo chafungwa

Marion Bosire
1 Min Read

Chuo kikuu cha Rongo katika kaunti ya Migori kimefungwa kwa muda usiojulikana kufuatia vurugu za wanafunzi zilizoshuhudiwa humo.

Kwenye taarifa naibu chansela wa chuo hicho anayehusika na masuala ya masomo na ya wanafunzi Michael Ntabo Mabururu alisema uamuzi wa kufunga chuo hicho uliafikiwa kwenye kikao cha seneti ya chuo hicho leo.

Wanafunzi wote wametakiwa kuondoka kwenye taasisi hiyo mara moja.

Vurugu hizo zinasemekana kuchochewa na kutoelewana kuhusu uchaguzi wa viongozi wa chama cha wanafunzi wa chuo hicho cha Rongo.

Makundi pinzani ya wanafunzi yalianza kukabiliana punde baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi hali iliyosababisha kuharibiwa kwa mali ya shule.

Reports indicate that opposing teams had engaged in a rampage following the announcement of the election results.

Baadhi ya wanafunzi waliwasha moto kwenye viwanja vya shule hiyo lakini hakuna waliojeruhiwa kwenye vurugu hizo.

Share This Article