Timu ya taifa ya Jamhuri ya Demokrasia maarufu kama The Leopards imejikatia tiketi kwa makala ya 35 ya fainali za AFCON mwaka ujao nchini Morocco.
Congo imefuzu Jumanne jioni baada ya kuwadhalilisha wenyeji Tanzania, mabao mawili kwa bila katika uwanja wa Mkapa.
Meshack Elia amepachika magoli yote mawili kwa wageni DRC, kunako kipindi cha pili.
Congo ambao ni wameshinda mechi zote nne wanaongoza kundi H kwa pointi 12.