Chui wa Congo amwangamiza Farao na kutinga robi fainali AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo maarufu kama Chui ,waliweka hai ya kutwaa ubingwa wa AFCON  baada ya subira ya miaka 50 baada ya kuwabandua Misri penati 8-7 Jumapili usiku.

Timu zote zilikuwa zimetoka sare ya bao moja baada ya dakika 120,Meshack Elia na Mostafa Mohammed wakifunga kipindi cha kwanza kwa Congo na Misri mtawalia.

Katika hatua ya matatua Misri walikosa mikwaju miwili ikiwemo ya mwisho kutoka kwa kipa Gbanski.

Chui wa Congo watakabiliana na tembo wa Guinea Ijumaa katika robo fainali .

Guinea ilifuzu kwa awamu ya nane bora baada ya kushinda derby ya Guinea walipoilaza Equatorial Guinea  bao moja kwa nunge.

 

Share This Article