Chosen Becky na Dictator Amir waachana.

Mtangazaji kwa jina Kasuku anasema Becky analaumiwa kwa visa kadhaa vya kutokuwa mwaminifu.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa Uganda Rebecca Kukiriza, maarufu kama Chosen Becky na mwanamitandao Dictator Amir wameachana kutokana na kile kinachotajwa kuwa ukosefu wa uaminifu katika uhusiano wao.

Utengano huo umedhibitishwa na Isaac Daniel Katende maarufu kama Kasuku, rafiki ya Chosen Becky, aliyesoma hewani jumbe alizosema alitumiwa za kudhibitisha ukosefu wa uaminifu.

Jumbe hizo zinaashiria kwamba Becky alikuwa na uhusiano wa kisiri wa kimapenzi na jamaa kwa jina Mathias Ssemanda, uhusiano wake na Amir, ukiendelea.

Amir ndiye alikutanisha Chosen Becky na Ssemanda, ili amsaidie kurejesha ukurasa wake wa Facebook ambao ulikuwa umedukuliwa.

Uhusiano huo wa kisiri kati ya Becky na Ssemanda, hata hivyo ulikatika punde baada ya Amir kujua.

Baada ya hapo mwanamuziki huyo anaripotiwa kuingilia uhusiano mwingine wa kisiri na meneja wa akaunti yake ya mtandao wa YouTube kwa jina Henry.

Kulingana na Kasuku, mkewe Henry alipata kufahamu na hivyo ikabidi wakatize.

Kasuku anasema Amir aliwahi kumkuta Becky na mpiga picha katika mazingira ya kutatanisha na wakati mwingine akampata na jamaa kwa jina Khadir.

Mtangazaji huyo anasema Becky aliwahi kumpigia simu akilia, akamwambia iwapo chochote kingemtokea, Amir awajibishwe.

Becky na Amir wana watoto watatu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *