China yashutumu mtazamo wa ‘poteza-poteza’ wa EU katika mzozo unaoongezeka wa kibiashara

Martin Mwanje
1 Min Read
Mao Ning - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China

China leo Ijumaa imeukosoa mtazamo wa “poteza-poteza” wa kibiashara unaochukuliwa na Umoja wa Ulaya, EU.

Hii ni baada ya mkuu wa umoja huo Charles Michel kusema kuwa China lazima “ibadilishe tabia yake” ili kusuluhisha mzozo unaoongezeka wa ushuru wa forodha na Ulaya.

“EU inapaswa kutambua bayana kuwa kuweka ushuru zaidi wa forodha hakutasuluhisha matatizo yoyote,” alisema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning.

Mao ametoa wito kwa EU “kuchukua hatua madhubuti na kufanya kazi pamoja na China kutafuta suluhu kupitia mazungumzo”.

Share This Article