China imeikosoa vikali Marekani kwa kupinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka mapigano huko Gaza kusitishwa mara moja.
Beijing inasema hatua hiyo ilituma “ujumbe mbaya” na kwa ufanisi ilitoa “mwanga wa kijani kwa uchinjaji unaoendelea”.
Ikulu ya White House ilisema azimio lililopendekezwa na Algeria “litahatarisha” mazungumzo ya kumaliza vita.
Marekani imependekeza azimio lake la kusitisha mapigano kwa muda, ambalo pia liliionya Israel kutouvamia mji wa Rafah.
Kumekuwa na shutuma nyingi kwa uamuzi wa Marekani wa kuzuia azimio la Algeria huku mapigano yakiendelea huko Gaza. Iiliungwa mkono na wanachama 13 kati ya 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa – huku Uingereza ikijizuia.
Akijibu kura hiyo ya turufu, Balozi wa China wa Umoja wa Mataifa Zhang Jun alisema madai hayo yataingilia mazungumzo ya kidiplomasia yanayoendelea “haiwezekani kabisa”.
“Kwa kuzingatia hali iliyopo, kuendelea kuepukwa kwa usitishaji mapigano mara moja sio tofauti na kusema mauaji yaendelee ,” alisema.
“Kusambaratika kwa mzozo kunavuruga eneo lote la Mashariki ya Kati na kusababisha kuongezeka kwa hatari ya vita vikubwa,” aliongeza.
“Ni kwa kuzima tu miale ya vita huko Gaza tunaweza kuzuia moto kuteketeza eneo lote.”
Mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Algeria alitangaza kuwa “kwa bahati mbaya Baraza la Usalama limeshindwa kwa mara nyingine tena”. “Chunguza dhamiri yako, historia itakuhukumu vipi,” Amar Bendjama aliongeza.
Washirika wa Marekani pia walikosoa hatua hiyo. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Ufaransa Nicolas de Rivière alielezea masikitiko yake kwamba azimio hilo halikupitishwa “licha ya hali mbaya inayoendelea.