Sehemu ya 1: Chimbuko la Michezo ya Olimpiki

Dismas Otuke
2 Min Read
Kipchoge Keino akishiriki mashidnanoni enzi zake

Michezo ya Olimpiki inayoandaliwa kila baada ya miaka minne ilianzia nchini Ugiriki kabla ya kufufuliwa tena katika karne ya 19.

Michezo hiyo iliwashirikisha wachezaji limbukeni pekee kabla ya mwaka 1970 na kisha kupanuliwa miaka 1980 kuwaruhusu wachezaji wengi wa kulipwa na fani nyingi za michezo.

Wachezaji wa kulipwa wa mpira wa kikapu na soka walishiriki fani 32 huku mashindano hayo yakiandaliwa msimu wa joto ili kuyatofautisha na ya msimu wa baridi.

Michezo ya Olimpiki ilikuwa maarufu sana nchini Ugiriki enzi hizo za kale ikiandaliwa kila baada ya miaka minne.

Kulingana na historia, michezo hiyo ilizinduliwa na Heracles mwanawe Zeus na Alcmene huku mpishi Coroebus kutoka Elis akiwa mshindi wa kwanza wa Olimpiki katika mbio za masafa mafupi miaka ya 776 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Kenya ilishiriki Olimpiki kwa mara ya kwanza mwaka 1956 mjini Melbourne, Australia ikiwakilishwa na wanariadha 25.

Hata hivyo, ni katika makala ya mwaka 64 ambapo Kenya ilishinda nishani ya kwanza ikiwa na shaba katika mita 800 kwa wanaume kupitia kwa marehemu Wilson Kiprugut Chumo.

Mwaka 1968 nchini Mexico, Kenya iliwakilishwa na wanamichezo 39 na kunyakua medali 9, zikiwemo 3 dhahabu, fedha 4 na shaba 2.

Marehemu Naftali Temu, akishinda dhahabu ya mita 10,000 mwaka 1968.

Marehemu Naftali Temu alikuwa Mkenya wa kwanza kushinda dhahabu ikiwa ya mita 10,000 ikisadifu kuwa dhahabu pekee kwa Wakenya katika mbio hizo.

Katika makala ya mwaka 1972 mnjini Munich, Ujerumani, Kipchoge Keino alinyakua nishani ya kwanza ya dhahabu ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji, akiwa Mkenya wa kwanza kunyakua dhahabu ya pili mtawalia baada ya kushinda dhahabu ya mita 1500 mwaka 1968.

Pia ni katika mashindano hayo ambayo Kenya ilishinda dhahabu ya kwanza ya mita 400 kwa wanariaha wanne kupokezana kijiti kwa wanaume, Robert Ouko, Julius Sang, Munyoro Nyamau na Charles Asati wakiwa katika kikosi hicho.

Website |  + posts
Share This Article