Chifu na msimamizi wa kijiji mahakamani kwa tuhuma za mauaji

Marion Bosire
1 Min Read

Chifu mmoja na msimamizi wa kijiji leo walifikishwa katika mahakama ya Meru kwa tuhuma za mauaji.

Nicholas Ikiugu chifu wa lokesheni ya Uruku na Paul Bundi anayesimamia kijiji cha Kiaruji village kilicho kwenye lokesheni hiyo walifikishwa mbele ya jaji wa mahakam kuu ya Meru Edward Muriithi.

Mahakama ilifahamishwa kwamba kati ya tarehe 2 na 8 Agosti mwaka 2022, wawili hao na wengine ambao hawakuwepo mahakamani walimuua Gedion Muchugu.

Washukiwa hawakupatiwa fursa ya kukiri au kukana mashtaka dhidi yao na badala yake jaji aliagiza wafanyiwe uchunguzi wa kiakili katika hospitali ya rufaa ya Meru kubaini iwapo wako sawa kuendelea na kesi.

Kesi hiyo itatajwa Agosti 8, 2024 kikao ambacho pa kitatumiwa kutoa uamuzi kuhusu ombi la washukiwa la kuachiliwa kwa dhamana.

Wawili hao kwa sasa wako rumande katika jela ya kuu ya Meru.

Share This Article