Bingwa wa dunia na Olimpiki katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji Faith Cherotich, atawaongoza Wakenya katika mkondo wa 14 na wa mwisho wa mashindano ya Diamond League ,Alhamisi usiku nchini Uswizi.
Cherotich ambaye ni wa pili kwa msimamo kwa pointi 28 atalenga kuchupa uongozini kwa kutumia fursa ya kukosekana kwa mpinzani wake wa jadi Winfred Yavi ambaye hatashiriki.
Bingwa wa Olimpiki Emmanuel Wanyonyi na mshindi wa nishani ya shaba ya Jumuiya ya Madola Wycliff Kinyamal watashiriki mita 800 zisizo za kuwania pointi.
Doris Lemongole ni Mkenya mwingine atakayetimka mbio hizo huku wate wawili wakiwania tiketi ya kufuzu kwa mkondo wa mwisho wa Brussels nchini Ubelgiji mwezi ujao.
Mshindi wa nishani ya fedha ya dunia Dorcas Ewoi atajitosa katika mita 1,500,pia akiwania tiketi kwa mkondo wa fainali utakaoandaliwa nchini Ubelgiji,akishikilia nafasi ya 4 kwa alama 5.
Bingwa wa Dunia mwaka 2019,Timothy Cheruiyot,na Phanuel Kosgei watapambana katika mita 1500.
Mkondo wa Alhamisi usiku utafuatwa na ule wa fainali utakaofayimka Brussels,Ubelgiji kati ya Septemba 4 na 5.